UCHAGUZI: MATOKEO YA AWALI ODINGA ANAONGOZA KWA ASILIMIA 52 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 13 August 2022

UCHAGUZI: MATOKEO YA AWALI ODINGA ANAONGOZA KWA ASILIMIA 52Mwanasiasa mkongwe wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga anaongoza kwa kura kidogo katika kinyang'anyiro cha kuwania urais dhidi ya naibu rais William Ruto. 


Kulingana na matokeo rasmi yaliyotolewa hadi sasa na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC, Odinga anaongoza kwa asilimia 52 na Ruto asilimia 46 ikiwa ni asilimia 30 ya kura zilizokwisha hesabiwa. 


Wakenya wanasubiri kwa hamu matokeo rasmi ya uchaguzi ikiwa ni siku tano baada ya kupiga kura siku ya Jumanne. 


Odinga mwenye umri wa miaka 77, anawania kiti hicho kwa mara ya tano na kuungwa mkono na rais anayeondoka madarakani Uhuru Kenyatta. 


Ruto mwenye miaka 55 amekuwa naibu rais kwa karibu muongo mmoja lakini aliwekwa kando baada ya mkono wa heri baina ya Odinga na Kenyatta mnamo mwaka 2018.

CHANZO:DW

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso