MCHUNGAJI MBARONI KWA TUHUMA ZA KULAWITI MTOTO MJINI SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 13 August 2022

MCHUNGAJI MBARONI KWA TUHUMA ZA KULAWITI MTOTO MJINI SHINYANGA

Shinyanga. Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikiria Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT), Makedonia ya Lubaga, Mjini Shinyanga, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka nane.


Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga (RPC), Janeth Magomi amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa jana Ijumaa Augosti 12, 2022 baada ya jeshi la Polisi mkoani humo kupokea malalamiko kutoka kwa moja ya familia za waumini wa kanisa hilo.


RPC Magomi amesema jeshi hilo linamshirikia mchungaji huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso