MAYELE ALETA KILIO SIMBA, YANGA MABINGWA NGAO YA JAMII 2022/23 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 13 August 2022

MAYELE ALETA KILIO SIMBA, YANGA MABINGWA NGAO YA JAMII 2022/23

 


Klabu ya Young Africans imefanikiwa kutwaa kombe la Ngao ya Jamii dhidi ya klabu ya Simba Sports Club kwa mwaka wa msimu 2022/2023.

Na Said Muhibu, Lango La Habari

Mchezo uliochezwa hii leo katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam uliwakutanisha watani wa jadi Yanga dhidi ya Simba na Yanga kufanikiwa kuifunga Simba mabao 2-1.


Simba ilitangulia kutikisa nyavu za Yanga kupitia Kiungo Mshambuliaji wake Pape Ousmane Sakho na kutamatika kwa kipindi cha kwanza Simba ikiwa kinara kwa bao 1-0.


Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko kwa Klabu ya Yanga, Jesus Moloko na Bernard Morrison wakiingia kuchukua nafasi za Sure Boy na Farid Mussa. Yanga ilifanikiwa kupindua meza kupitia Mshambuliaji wake Fiston Kalala Mayele ambaye aliingia nyavuni mara mbili na kufanikiwa kuipatia Yanga ubingwa huku mchezo ukitamatika kwa Yanga kushinda magoli 2-1.


Hadi hivi sasa klabu hizo mbili zimekutana mara 105 huku Yanga ikipata ushindi mara 38 na Simba 28 na wakitoa sare mara 42.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso