MWANAMKE ALIWA MAMBA KUTOKANA NA ADHA YA MAJI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 16 August 2022

MWANAMKE ALIWA MAMBA KUTOKANA NA ADHA YA MAJI

Ombwe la kutomtua ndoo kichwani mwanamke,imesababisha majonzi katika Kijiji cha Kipingu,Halmashauri ya Ludewa mkoani Njombe,kufuatia  Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Orester Haule (25)  kufariki dunia baada ya kukamatwa na mamba  na kumzamisha kwenye Maji  wakati akichota maji katika mto Ruhuhu kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.



Mama huyo ameacha watoto wawili wadogo na kuzua simanzi kubwa katika jamii inayowazunguka watoto hao inayojadili mustakabari wa maisha ya vijana hao.


Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kipingu Alphonce Mbeya anasema tukio hilo limetokea Agosti 13 majira ya saa 12 jioni wakati mwanamke huyo akiwa na wenzake wakifata huduma ya maji kwa matumizi ya nyumbani  ambapo inaelezwa hadi tukio hilo limetokea tayari watu 4 wameshambuliwa na mamba wakisaka maji.


Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ludewa wamelazimika kufika msibani kuwapa pole wafiwa na kisha kuahidi kutatua changamoto ya mradi wa maji katika kijiji hicho huku pia wakitoa agizo kwa wizara ya mali asili na utili kuwavuna mamba katika mto huo ili kunusuru vifo vinavyoweza kuzuilika.

CHANZO:EATVNEWS

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso