AFISA TUME YA UCHAGUZI KENYA AKUTWA MSITUNI AKIWA AMEFARIKI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 16 August 2022

AFISA TUME YA UCHAGUZI KENYA AKUTWA MSITUNI AKIWA AMEFARIKI

 


Mwili wa Ofisa wa Tume Huru ya uchaguzi na Mipaka ( IEBC ) ya Kenye,Daniel Musyoka (53), aliyepotea akiwa kituo cha kupigia kura na kuzua sintofahamu,umepatikana katika msitu wa Kilombero nchini humo,ukiwa umepoteza uhai,ikiwa ni saa chache tangu tume hiyo  kumtangaza Dk William Ruto kuwa Rais mteule wa Kenya.


Ofisa huyo, Musyoka  alikuwa msimamizi wa Kaunti ya Embakasi Mashariki iliyopo katika jiji la Nairobi na mwill wake umepatikana jana, Jumatatu Agosti 15, 2022 katika msitu eneo la Kajiado.


Akizungumzia kupatikana kwa mwili huo, Ofisa wa Polisi wa Loitoktok, Kipruto Ruto, amesema walipewa taarifa za kuwapo kwa mwili huo ambao baadaye dada zake waliutambua mwili huo ni wa ndugu yao.


CHANZO:MILLARD AYO

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso