NANE WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI MBEYA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 16 August 2022

NANE WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI MBEYA




Watu nane wamefariki dunia na wengine ambao idadi yao haijafahamika wakijeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea leo Jumanne, Agosti 16, 2022 eneo la Shamwengo karibu na kituo cha mafuta Inyala mkoani Mbeya.


Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani humo, Urlich Matei amethibitisha kutokea tukio hilo akisema gari kubwa lililokuwa limebeba kontena la mchanga lilifeli breki na kuligonga basi la Super Rojas lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Njombe.


Amesema baada ya kugonga basi hilo, liliendelea kushuka zaidi na kuligonga gari lingine lenye aina ya benzi na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa ambao idadi yao haijajulikana haraka.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso