KIAPO KINZANI CHAKOSEWA JINA KWA MAKUSUDI AU SIO KWA MAKUSUDI-WAKILI AKINA MDEE AELEZA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 26 August 2022

KIAPO KINZANI CHAKOSEWA JINA KWA MAKUSUDI AU SIO KWA MAKUSUDI-WAKILI AKINA MDEE AELEZA



Wakili wa waleta maombi wa mbunge Halima Mdee na wenzake saba, Ipilinga Panya ameieleza Mahakama kuu, Masjiala Kuu kuwa kiapo kinzani kilichowasilishwa na Chadema kimekosewa jina eidha kwa makusudi au kukusudia.


Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Chadema Peter Kibatala kuwasilisha ombi mbele ya Jaji Cyprian Mkeha kuwa atoe hati ya wito kwa wabunge hao ili waje kuwahoji mahakamani hapo kuhusiana na viapo vyao. 


Mbali na Mdee wabunge wengine ni Grace Tendega, Esther Matiko, Esther Bulaya, Cecilia Pareso, Hawa Mwaifunga, Jesca Kishoa na Nusrat Hanje. 


Panya ameieleza Mahakama hiyo kuwa kiapo kinzani hicho kimeandikwa kwa jina la bodi ya wadhamini ambalo wao wenyewe Chadema walilikataa kwenye maombi ya awali namba 16 ya mwaka 2022 yaliyotupiliwa mbali na jaji John Mgeta. Amesema hoja hiyo ni hoja ya kisheria Mahakama hiyo inapaswa kusikiliza Kwanza kabla ya kuanza kusikiliza kwa shauri la msingi. 


Kwa upande wa wakili wa Serikali wa wajibu maombiwa Tume ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Stanley Kalokola amesema wao hawajawasilisha kiapo Kwa kuwa hakuna kinachowahusubisipokuwa wametekeleza amri ya kimahakama.


Naye wakili wa wajibu maombi Peter Kibatala amesema waleta maombi njia waliotumia kuwasilisha maombi yao haiko Sawa badala yake walitakiwa waombe mapitio ya mahakama hivyo anaona hoja yao haina msingi itupiliwe mbali Kwa gharama yeyote. 


Baada ya kusikiliza hoja za pande zote Jaji Cyprian Mkeha amehirisha shauri hilo Hadi Septemba 2 Kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso