AJALI YA MAGARI MATATU YAUA WATU 20 NA MAJERUHI 15-KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 9 August 2022

AJALI YA MAGARI MATATU YAUA WATU 20 NA MAJERUHI 15-KAHAMA




Watu 20 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha magari matatu na Trekta katika eneo la Mwakata barabara ya Isaka Kahama mkoani Shinyanga.


Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo imetokea majira ya saa nne usiku Jumatatu Agosti 8,2022 ikihusisha gari ndogo IST yenye namba za usajili T880 DUE, Hiace yenye namba za usajili T350 BDX, Lori na Trekta. Inaelezwa kuwa Hiace imegongana uso kwa uso na Lori/Scania yenye namba za usajili T658 DUW.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hospitali ya Kahama watu 20 wamepoteza maisha na 15 kujeruhiwa katika ajali hiyo na majeruhi wanaendelea kupata matibabu.


"Watu 17 walipoteza maisha papo hapo eneo la tukio na watatu wamefariki baada ya kufikishwa hospitali,majeruhi wapo 15", taarifa inaeleza.


Mpaka sasa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga halijazungumzia kuhusu tukio hili,juhudi za kumtafuta Kamanda wa polisi zinaendelea.


Habari hii kutoka Malunde 1 blog

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso