MIILI SABA KATI YA 20 WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA GARI KAHAMA YATAMBULIWA NA NDUGU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 9 August 2022

MIILI SABA KATI YA 20 WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA GARI KAHAMA YATAMBULIWA NA NDUGUJumla ya majeruhi 18 na miili 17 ya marehemu imepokelewa Agosti 08, 2022 majira ya usiku katika hospitali ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga baada ya ajali ya magari manne kugongana maeneo ya Isaka.


NA TAIKILE TURO-HUHESO DIGITAL


Akizungumza na HUHESO fm leo Agosti 09, 2022 mganga mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama, Deogratius Nyaga amesema kati ya majeruhi 18 waliowapokea, majeruhi watatu walifariki wakiwa katika chumba cha dharura hivyo kufikia idadi ya walifariki kutokana na ajali hiyo 20.


Amesema zoezi la ndugu kutambua marehemu linaendelea ambapo mpaka sasa jumla ya marehemu saba wametambuliwa na ndugu zao huku miili 13 ikiwa bado haijatambuliwa.


Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Henry Mwaibambe aliyefika eneo la tukio amesema ajali hiyo ilitokea Agosti 8, 2022 Majira ya saa nne kasoro usiku katika kijiji cha Mwakata kata ya Mwakata wilaya ya Kahama.


MWISHO

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso