MBOLEA KUSHUKA BEI KUANZIA AGOSTI 15-RAIS SAMIA AWATAKA VIJANA KUINGIA KWENYE KILIMO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 8 August 2022

MBOLEA KUSHUKA BEI KUANZIA AGOSTI 15-RAIS SAMIA AWATAKA VIJANA KUINGIA KWENYE KILIMO

 


Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza mpango wa ruzuku ya pembejeo aliozindua leo uanze kutekelezwa Agosti 15 mwaka huu ili kuwawezesha wakulima kujipanga na msimu mpya wa kilimo.


Akizungumza leo Jumatatu Agosti 8, 2022 wakati wa maadhimisho ya siku ya wakulima jijini Mbeya, Rais Samia amemuelekeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba kuhakikisha fedha za utekelezaji wa mpango huo zinatolewa kwa haraka.


Amesema, ‘’Waziri wa fe sha umeniambia fedha ziko tayari ila kuna taratibu zinatakiwa zitimie, lakini nataka niseme kwamba ruzuku hizi zianze kuanzia Agosti 15 ili wakulima wajitayarishe kuanza msimu unaokuja,”.


Mpango huo wa ruzuku utawezesha wakulima kupata nafuu ya bei ya mbolea hatua itakayowasaidia kuwapunguzia mzigo.


Waziri wa Kilimo Hussen Bashe amesema mpango huo unafanya bei ya mbolea ya DAP kuuzwa Sh70,000 kutoka Sh131,000 huku bei ya Urea ikifikia Sh70,000 kutoka Sh124,734.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso