MKUNGA ALIETELEKEZA MAMA MJAMZITO ASIMAMISHWA KAZI-KAGERA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 2 July 2022

MKUNGA ALIETELEKEZA MAMA MJAMZITO ASIMAMISHWA KAZI-KAGERA



Mkunga wa zahanati ya Kashai iliyopo Manispaa ya Bukoba, Leticia Muganyizi amesimamishwa kazi kwa kipindi cha miezi mitatu na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania kwa kosa la kutelekeza akina mama wajawazito.


Tukio hilo lililotokea jana Julai Mosi, 2022 limesababisha adha kwa wajawazito hao na hivyo kukiuka sheria ya uuguzi na ukunga yam waka 2010 kifungu cha 25 (2)(a) na (3)(f)(k) pamoja na kanuni na misingi ya maadili ya kitaaluma ya wauguzi na wkaunga Tanzania kwamba ni marufuku kumtelekeza mgonjwa, mgonjwa anapaswa kupata huduma salama, zenye ubora na staha.


Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Juni 2 na Msajili wa Baraza hilo, Agnes Mtawa imeeleza kuwa mkunga huyo pamoja na mhudumu walikataa kuwafungulia mlango akina mama wajawazito wawili waliofika kujifungua usiku kwa madai ya kuhofia usalama wao.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso