NAULI ZA MV VICTORIA ZAPANDA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 2 July 2022

NAULI ZA MV VICTORIA ZAPANDA




Uongozi wa kampuni ya huduma za meli (MSCL) umetangaza kupanda kwa nauli meli za MV Victoria na MV Butiama, kuanzia Julai 4 mwaka huu.


  Na Abela Msikula, Mwanza


Kiwango kipya cha nauri kwa MV Victoria ni Sh21,000 kwa daraja la tatu (Uchumi), kutoka Sh16,000 za awali.


Daraja la pili (Biashara) nauli mpya ni Sh.40,000 kutoka Sh.30,000 ya awali, amesema Afisa Habari wa Kampuni, Abdulrahman Salimu.


"Na kwa daraja la kwanza, nauli ya awali ilikuwa Sh45,000 na sasa imekuwa Sh 55,000. Nauri zote hizi ni kwa watu wazima wenye umri kuanzia miaka 12,"amesema na kufafanua zaidi kwamba: Watoto wa umri kuanzia miaka mitano hadi 11 watakua wakilipa nusu ya nauri husika kwa kila daraja.


Kwa upande wa MV Butiama yenye madaraja mawili tu, uchumi na biashara, nauli kuongezeka kwa Sh. 2,000.


Daraja la uchumi nauli ilikuwa Sh8,000 na sasa itakua Sh10,000 wakati daraja la biashara nauli ilikuwa Sh10,000 na sasa itakua Sh12,000.


Chanzo:Habari leo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso