BEAKINGNEWS: SOPU APIGA TATU YANGA IKITWAA UBINGWA WA FA CUP 2021/22 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 2 July 2022

BEAKINGNEWS: SOPU APIGA TATU YANGA IKITWAA UBINGWA WA FA CUP 2021/22






NA PASCHAL MALULU-HUHESO DIGITAL


Mshambuliaji wa kikosi cha Coastal Union maarufu (wagosi wa Kaya) Abdul Seleman maarufu Sopu amefanikiwa kufunga mabao matatu(HATTRICK) katika mchezo wa fainali wa michuano ya Azam Sports federation Cup Tanzania bara uliochezwa jijini Arusha.


Katika mchezo huo wa fainali kati ya Coastal Union dhidi ya Yanga timu hizo zimefanikiwa kutoka sare ya kufungana mabao 3-3 ambapo mabao ya Yanga yakifungwa na Salum Abdalah (Fei Toto) bao la pili likifungwa na mshambuliaji mkongomani Makambo na bao la tatu la Yanga likifungwa na Denis Nkane na kukamilisha dakika 120 kwa kufungana mabao 3-3 ambapo dakika 90 zilimalizika kwa kufungana mabao 2-2 na kuongezwa dakika 30.


Mikwaju ya penati Yanga wamefanikiwa kufunga penati 4 na Coastal Union wakifunga Penati 1 pekee.


Mfungaji bora wa michuano hiyo ni Abdul Seleman Sopu ambapo amefikisha jumla ya mabao 9.






No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso