KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA NYAMA YA KASA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 20 July 2022

KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA NYAMA YA KASA




Mkazi wa Msanga Mkuu, Ally Hassan, (46) amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Mtwara kwa makosa mawili ya kukutwa akivua maeneo yaliyokatazwa na kukutwa na nyama ya kasa.

Na Mwanamkasi Jumbe

Mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo, Mussa Esanju, Mwendesha mashitaka wa Serikali , Gideon Magesa ameieleza mahakama hiyo kuwa mnamo Mei 14, 2022 mshtakiwa alikutwa akivua katika eneo linalokatazwa kufanya shughuli za uvuvi.


Vile vile Mshtakiwa huyo alikutwa na nyama ya kasa kinyume cha sheria na kanuni za uvuvi.


Mshtakiwa huyo amekana kosa na kesi imeahirishwa hadi Agosti 2 mwaka huu.


Hakimu Esanju ameiambia Mwananchi digital leo Julai 20, 2022 kuwa shitaka hilo litafikishwa tena mahakamani hapo kwa ajili ya kusoma na kuchambua kwa sababu upelelezi umekamilika.


Hakimu Esanju amesema ameelekeza kwamba hati ya mashtaka ifanyiwe marekebisho ili ionyeshe uzito wa nyama aliyokutwa nayo mshtakiwa huyo ili pia kujua thamani yake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso