AJIUA BAADA YA MKE WAKE KUSUSIA KURUDIANA NAE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 20 July 2022

AJIUA BAADA YA MKE WAKE KUSUSIA KURUDIANA NAE





Mwanaume mmoja alijiua ka kujipiga risasi eneo la Muthangari jijini Nairobi baada ya mke wake waliyekosana kukataa kumrudia.


Iyaz Mukhi mwenye umri wa miaka 63 alienda kwa nyumba ya mwanamke huyo ambaye walikosana na kutengana Septemba mwaka jana kwa sababu za kinyumbani.


Lengo kuu la mfanyabiashara huyo lilikuwa kumshawishi mkewe amrudie, na alianza kwa kuomba msamaha na kuendelea kumrai mama wa watoto wake wawili kumrudia lakini rai zake ziligonga mwamba.


Baada ya ombi lake kukataliwa, Mukhi alichomoa bastola yake aina ya Glock na kujipiga risasi katika nyumba ya mwanamke huyo huku waliokuwepo wakikimbia kwa kuhofia usalama wao.


“Mke wake alipokataa kumsamehe, alichomoa bastola na kujipiga risasi. Bastola ya Glock na vazi la risasi moja iliyotumika vilipatikana eneo la tukio,” taarifa ya polisi inasema. Kwa mujibu wa polisi, mwendazake alikuwa na leseni ya kumiliki bunduki na bastola aliyokuwa nayo ilikuwa na risasi 12. Polisi anasema kuwa wanachunguza kisa hicho na watanakili taarifa kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo mashahidi.


Mwili wake ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ambako unatarajiwa kufanyiwa upasuaji mnamo leo Jumatano, Julai 20,2022.


Visa vya watu kujitoa uhai vinazidi kuongezeka huku polisi wakirekodi angalau visa viwili kila siku.


Mwaka 2019, watu 499 walijitoa uhai huku watu 575 wakijiua mwaka 2020. Japokuwa polisi wangali kutoa takwimu za mwaka huu, inaripotiwa kuwa watu 313 wamejitoa uhai kati ya Januari na Julai 2022.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso