KESI YA SABAYA NA WENZAKE YAPIGWA KALENDA TENA SABABU YATAJWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 4 July 2022

KESI YA SABAYA NA WENZAKE YAPIGWA KALENDA TENA SABABU YATAJWA





Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi imeahirisha tena kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne kutokana na upelezi kutokamilika.


Sabaya na wenzake leo Julai 4, 2022 wamefikishwa kwa mara ya nne katika mahakama hiyo kujibu tuhuma zinazowakabili katika kesi namba 2 ya uhujumu uchumi ya mwaka 2022 lakini kesi hiyo imeahirishwa tena.


Kesi hiyo inayoendeshwa na wakili wa upande wa Jamuhuri, Kasimu Daudi pamoja na Sabitina Mcharo imehairishwa hadi hapo Julai 14, 2022 kutokana na upelezi wa kesi hiyo kutokamilika.


Wakili wa Serikali Kasimu Daudi ameieleza mahakama hiyo kuwa bado upelelezi haujakamilika na pia wanasubiri hati ya kuipa mahakama hiyo uwezo wa kuisikiliza kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso