MIILI SITA YA WANAFAMILIA ILIYOUAWA YAZIKWA KWA PAMOJA USIKU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 4 July 2022

MIILI SITA YA WANAFAMILIA ILIYOUAWA YAZIKWA KWA PAMOJA USIKU



Miili ya watu sita wa familia moja waliouawa kwa kukatwa na kitu chanye ncha kali na watu wasiojulikana imezikwa katika Kijiji cha Kiganza, wilayani Kigoma mkoani Kigoma.


Miili hiyo imezikwa kwa pamoja jana Jumapili Julai 3, 2022 usiku.


Watu hao waliuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana wakiwa nyumbani kwao wamelala huku watoto wawili, mmoja mwenye umri wa miezi mitatu na mwingine miaka minne wakijeruhiwa.


Jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Menrad Sindano alithibitisha mauaji hayo huku akisema kuwa Jeshi hilo limeanza msako wa waliofanya unyama huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso