UAMZI KESI YA MFALME ZUMARIDI WAKWAMA KUTOLEWA SABABU ZATAJWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 18 July 2022

UAMZI KESI YA MFALME ZUMARIDI WAKWAMA KUTOLEWA SABABU ZATAJWA




Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza imeshindwa kutoa uamuzi mdogo wa maombi ya upande wa utetezi yaliyomtaka hakimu anayesikiliza kesi hiyo ya jinai namba 10/2022, Monica Ndyekobora kujiondoa kusikiliza kesi hiyo kwa kile ulichodai hauna imani na hakimu huyo.


Julai 11 mwaka huu, mshtakiwa namba moja katika kesi hiyo yenye mashtaka matatu ikiwemo kushambulia na kuzuia maofisa wa umma kutekeleza majukumu yao, Diana Bundala maarufu kama "Mfalme Zumaridi" kupitia kwa wakili wake, Steven Kitale akisaidiana na Erick Mutta aliiambia mahakama hiyo kwamba hana imani na hakimu anayesikiliza kesi hiyo huku akimtaka kujiondoa.


Akizungumza leo Julai 18, 2022 ndani ya chumba cha mahakama hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Emmanuel Luvinga ameiambia mahakama hiyo kwamba kesi hiyo imeitwa leo kwa ajili ya kutolewa uamuzi mdogo kuhusu maombi yaliyowasilishwa na mshtakiwa namba moja kwa hakimu huyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso