SERIKALI YAHOJI WANANCHI KUTOKUANDIKA WOSIA (RITA WATAKIWA KUTOA ELIMU) - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 18 July 2022

SERIKALI YAHOJI WANANCHI KUTOKUANDIKA WOSIA (RITA WATAKIWA KUTOA ELIMU)



Wizara ya Katiba na Sheria imeilekeza Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) kukusanya maoni kwa wananchi ili kubaini sababu zinazofanya kuwa na mwitikio mdogo katika kuandika wosia.


Katibu Mkuu wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo amesema ipo haja kwa Serikali kutambua kiini cha hali hiyo na kuona namna ya kutatua ili kupunguza migogoro ya mirathi ambayo kwa kiasi kikubwa waathirika ni wanawake na watoto.


Akizungumza leo wakati wa mkutano wa mamlaka hiyo na wadau Mary amesema licha ya hamasa kubwa kutolewa kuhusu umuhimu wa wosia mi watanzania wachache ambao tayari wameandika wosia.


“Tunawaelekeza Rita kuandaa dodoso ipelekwe kwa wananchi waeleze sababu zinazofanywa washindwe kuandika wosia, tumefika huku maana migogoro imekuwa mingi ambayo ingeweza kuzuilika.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso