YANGA SC YATWAA UBINGWA WA LIGI KUU 2021/22 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 15 June 2022

YANGA SC YATWAA UBINGWA WA LIGI KUU 2021/22

KLABU ya Yanga imefanikiwa kunyakuwa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara mara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Coastal Union.

255715292924_status_87c9ca1a5fa84ce59f1b48622e207052

Yanga Sc ilikuwa inahitaji pointi tatu ambazo zingeifanya isifikiwe na timu yoyote ile kwa michezo iliyosalia ya kigi kuu ya NBC.


Mabao ya Yanga yamewekwa kimyani na mshambuliaji wao Fiston Kalala Mayele ambaye alipachika mabao mawili katika dakika ya 34 na 67 na bao lingine likifungwa na Chiko Ushindi katika dakika ya 51.


Mayele sasa ataendelea kuongoza ufungaji bora akiwa na mabao 16 akifuatia na mshambuliaji wa Geita Gold George Mpole.



Timu ya Yanga sasa imefikisha ubingwa wa ligi kuu mara ya 28 tangu kuchukua ubingwa huo 2016/2017.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso