WALIOMUUA MWANAFUNZI WA CHEKECHEA WAFIKISHWA MAHAKAMANI-GEITA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 22 June 2022

WALIOMUUA MWANAFUNZI WA CHEKECHEA WAFIKISHWA MAHAKAMANI-GEITA


Watuhumiwa watatu waliotambuliwa kwa majina ya Sitta Makabila wa miaka 52 mkazi wa Kilimanjaro ambaye ni mganga wa kienyeji, Mathias Shilole (26) mkulima na Lucy Mlelema wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji.


Watuhumiwa hao wanatuhumiwa kufanya mauaji ya mtoto mwenye umri wa miaka saba mwanafunzi wa chekechea katika shule ya msingi Ibambila wilayani Nyang’hwale mkoani Geita.


Akizungumza na wandishi wa habari kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Geita, Henry Mwaibambe amesema watu hao walimvamia binti ambaye alikuwa akichunga mbuzi na wenzie kisha kuchukuliwa na watu hao.


Amesema watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani Jana Juni 21, 2022.


Kamanda Mwaibambe amesema watuhumiwa kabla ya kutekeleza maujai hayo walimbaka mtoto huyo na kumlawiti kisha kumuua.

chanzo:Millardayo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso