MGANGA WA KIENYEJI ALIEHUSIKA NA VIUNGO VYA BINADAMU AHUKUMIWA MIAKA 10-KIGOMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 21 June 2022

MGANGA WA KIENYEJI ALIEHUSIKA NA VIUNGO VYA BINADAMU AHUKUMIWA MIAKA 10-KIGOMA






Jeshi la polisi mkoani Kigoma limesema mtuhumiwa mmoja ambaye alikuwa ni mganga wa kienyeji Mathayo Ndayishimiye ambaye ni kati ya watuhumiwa tisa waliokamatwa kwa tuhuma za kusafirisha viungo vya Binadamu amehukumiwa miaka 10 jela.


Mbali na kifungo hicho mganga huyo bado anakabiliwa na kesi nyingine ambayo bado inaendelea ikihusisha viungo vingine vya binadamu wilayani Buhigwe mkoani humo.


Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Kigoma, James Manyama amezungumza na vyombo vya habari akithibitisha kuwa mganga huyo alikiri kosa hivyo kukutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo hicho huku wengine wakiendelea kujibu mashtaka dhidi yao.


Chanzo:Millardayo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso