MGAHAWA WA MIAKA HAMSINI WAZAMA BAHARINI HUZUNI YATANDA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 21 June 2022

MGAHAWA WA MIAKA HAMSINI WAZAMA BAHARINI HUZUNI YATANDA





Mgahawa unaoelea ambao ulikuwa alama maarufu ya Hong Kong umezama siku chache baada ya kuvutwa kutoka bandarini ambako ulifanya kazi kwa takriban miaka 50.


Mgahawa wa Jumbo ulitumbukia katika Bahari ya Kusini ya China wakati ukielekea eneo lisilojulikana, kampuni mama inayomiliki mgahawa huo ilisema.


Kampuni ya Aberdeen Restaurant Enterprises ilisema "imehuzunishwa sana na tukio hilo" lakini hakuna wafanyakazi waliojeruhiwa.


Mgahawa huo ulifungwa Machi 2020 wakati janga la Covid-19 liliposhamiri.


Zaidi ya wageni milioni 3 wanaaminika kula vyakula vyake kwa miaka mingi, wakiwemo Malkia Elizabeth, Tom Cruise na Richard Branson.


Pia umeangaziwakatika filamu kadhaa ikiwa ni pamoja na filamu ya Bond - lakini janga la corona lilifanya biashara hiyo kuwa mbaya zaidi baada ya wageni kutotembelea tena.


Meli hiyo ilipaswa kukaa katika eneo lisilojulikana huku ikisubiri mwendeshaji mpya.


Lakini ilizama siku ya Jumapili karibu na Visiwa vya Paracel baada ya "kukabiliana na hali mbaya" na kuanza kuingiza maji, Aberdeen Restaurant Enterprises ilisema.

Chanzo:bbc

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso