CHADEMA NA WABUNGE WAO 19 KUCHUANA MAHAKAMANI LEO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 13 June 2022

CHADEMA NA WABUNGE WAO 19 KUCHUANA MAHAKAMANI LEO


Makada wa zamani 19 wa Chadema na wabunge wa viti maalumu, waliovuliwa uanachama wa chama hicho, Halima Mdee na wenzake 18, leo wanatarajiwa kuchuana vikali kwa hoja za kisheria na chama hicho mahakamani wakati maombi yao yatakaposikilizwa.


Mdee na wenzake wamekwenda mahakama kupinga uamuzi wa chama hicho kuwavua uanachama na wamefungua maombi Mahakama Kuu, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema, wakiomba kibali cha kufungua shauri la mapitio ya kuhusu uamuzi huo.


Sambamba na maombi hayo, pia wamefungua maombi ya zuio la muda dhidi ya ubunge wao kusubiri usikilizwaji na uamuzi wa maombi yao ya kibali cha kufungua kesi.


Maombi hayo yote yamepangwa kusikilizwa leo na Jaji John Mgetta na mawakili wa pande zote watachua kwa hoja za kisheria.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso