PANYA KALOWA WAIBUKA DODOMA NI KAMA "PANYAROAD" SERIKALI YATOA OMBI KWA WANANCHI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 13 June 2022

PANYA KALOWA WAIBUKA DODOMA NI KAMA "PANYAROAD" SERIKALI YATOA OMBI KWA WANANCHI


Mbunge wa Viti Maalum, Fatuma Toufiq ameibua sakata la kikundi cha uhalifu maarufu Panya Kalowa ambacho amesema kinawasumbua wananchi wa Kata ya Dodoma Makulu jijini Dodoma.


Toufiq ametoa kauli hiyo wakati akiuliza swali la nyongeza bungeni leo Jumatatu Juni 13, 2022 ambapo amesema kuwa kumeibuka kikundi hicho kinachoumiza wananchi.


“Mheshimiwa Naibu Spika kumeibuka kikundi kinachoitwa panya kalowa ambacho kinaumiza watu, nataka kujua Serikali inachukua hatua gani kudhibiti kikundi hicho ambacho ni hatari kwa wananchi,” amehoji Toufiq.


Swali la mbunge huyo limekuja huku kukiwa na matukio mengi ya ukabaji na mauaji yanayoripotiwa katika maeneo kadhaa ya Jiji la Dodoma huku Kata za Chang’ombe na Dodoma zikiongoza kuwa na matukio mengi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso