MORRISON WA SIMBA APEWA MAPUMZIKO YA JUMLA SIMBA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 13 May 2022

MORRISON WA SIMBA APEWA MAPUMZIKO YA JUMLA SIMBA












Klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam imempa mapumziko ya hadi mwisho wa msimu mchezaji wake Bernad Morrison.


Simba imefikia maamuzi hayo baada ya pande zote mbili kukubaliana kwa lengo la kumpa nafasi Morrison kupumzika na kushughulikia mambo yake binafsi na taarifa hiyo pia imesema inamshukuru kwa mchango wake ndani ya klabu yake.


Taarifa ya Simba imesema inatambua na kuthamini mchango wa Morrison katika kipindi cha miaka miwili alichohudumu ndani ya klabu ya Simba na kuisaidia kufika hatua ya robo fainali ya michuano ya Africa mara mbili, kuchukua ubingwa wa ligi kuu, kombe la mapinduzi na ubingwa wa Azam sports federation.


Simba imesema kwa mchango na mafanikio hayo klabu inamshukuru mchezaji huyo kipenzi cha mashabiki wa klabu hiyo kwa kujitoa kuipigania klabu yake hivyo inamtakia mapumziko mema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso