KITENGO MAALUM CHA UTALII NA DIPLOMSIA CHAANZISHWA NA JESHI LA POLISI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 13 May 2022

KITENGO MAALUM CHA UTALII NA DIPLOMSIA CHAANZISHWA NA JESHI LA POLISI




Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo kwa niaba ya Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania amesema Polisi wameanzisha kitengo maalumu cha Utalii na Diplomasia.


Amesema kitengo hicho kipo kwa ajili ya kuwahudumia Watalii na Wanadiplomasia wanaofika Tanzania, hii ni baada ya Mhe. Rais Samia kuzindua filamu ya Royal Tour.


Kamanda Masejo amesema kwa Mkoa wa Arusha ambao ni kitovu cha utalii nchini kumeanzishwa kituo cha Polisi maalumu kwa ajili ya kuhudumia Watalii na Wanadiplomasia ambapo Askari wake wamepatiwa mafunzo ndani na nje ya Nchi kuhusu namna bora ya kuhudumia Watalii.


Pia amesema kuwa kuna magari maalumu ambayo hutumiwa na kituo hicho kwa ajili ya doria mbalimbali ikiwemo kwenye vivutio vya utalii, hoteli za kitalii pamoja na maeneo mengine ambayo wageni hupenda kutembelea.


Sambamba na hilo kuna vituo vidogo vya Polisi vilivyopo katika Wilaya ya Arumeru, Monduli, Longido na Karatu ambapo magari ya utalii hufika kwa ajili ya kupata taarifa za kitalii pamoja na ukaguzi wa usalama wa magari hayo.


 "Jeshi la Polisi litaendelea kumuunga mkono Rais wa Samia katika kuutangaza utalii kwa kuboresha mazingira ya kiusalama kwa Watalii".

CHANZO:MILLARDAYO

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso