WAZIRI MULAMULA AFANIKISHA UJENZI WA BWENI LA WASICHANA MINZIRO. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 2 January 2022

WAZIRI MULAMULA AFANIKISHA UJENZI WA BWENI LA WASICHANA MINZIRO.

 

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Liberata Mulamula alipowasili Minziro Wilayani Misenyi Mkoani Kagera.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Liberata Mulamula alipowasili Minziro na kusalimiana na viongozi mbalimbali katika Sherehe za Kuchangia bweni la Wasichana katika Shule ya Minziro Sekondari Wilaya ya Misenyi, Mkoani Kagera.


WAKAZI wa Kata ya Minziro,Jimbo la Nkenge,wilaya ya Missenyi, mkoani Kagera wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Liberata Mulamula wamefanikisha kupatikana kwa kiasi cha Shilingi Milioni 12.7 katika Harambee ya kuchangia Bweni la wasichana.


Kiasi hicho cha fedha kimelekezwa kwa ajili ya shughuli za Maendeleo katika sekta ya Elimu,Katani hapo,hususani ujenzi huo wa bweni ili kuhakikisha wasichana wanasoma kwa utulivu na kufanya vyema katika masomo yao.

 

Harambee hiyo iliyofanyika mwishoni mwa siku za kufunga mwaka na kuhudhuriwa na mgeni rasmi,Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Liberata Mulamula,kilipatikana kiasi hicho na kukielekeza sekta ya elimu Sekondari.

 

Katika harambee hiyo,ambayo Balozi Mulamula,alichanga kiasi cha Shilingi Milioni Mbili, zilipatikana Shilingi milioni Mbili, Laki Saba na elfu sabini na tisa ( 2,779,000/-) zikiwa pesa taslimu,Shilingi Milioni Kumi na Elfu Ishirini ( 10,020,000/-) ahadi, huku mchanga ukiwa tripu 15 na mawe tripu sita.

 

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Liberata Mulamula akiweka jiwe la Msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Bweni la Wasichana katika shule ya Sekondari Minziro, Wilayani Misenyi, Mkoa wa Kagera.


Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Liberata Mulamula akitoa hotuba yake kwa wananchi wa Minziro kwenye kuchangia bweni la Wasichana katika Shule ya Minziro.

Akiongea neno la utangulizi kabla ya kufanyika harambee hiyo,Mratibu wa shughuli hiyo,ijulikanayo kwa jina la “Minziro Day”,Novath Rukwago,alisema chimbuko lake linatokana na wazaliwa wa Kata hiyo, wanaoishi na kufanya shughuli mbalmbali katika maeneo kadhaa ya nchini na nje ya nchi.

 

Rukwago alisema shughuli hiyo itakuwa endelevu kila mwaka kwa tarehe na mwezi, lengo likiwa ni kukutana na kushirikisha mawazo baina yao na wakazi wa kata hiyo kwa kubainisha changamoto zinazokabili kata na kuzipatia ufumbuzi utakaokuwa chachu ya kujipatia Maendeleo.

 

“ Na baada ya kushirikishana na ndugu zetu wanaoishi katika Kata hii, tukaona tuanze na changamoto ya kutatua katika sekta ya elimu sekondari kwa kuchangia ujenzi wa bweni  la wasichana Sekondari ya Minziro,”alisema Rukwago.


Mratibu wa shughuli kwa jina la “Minziro Day”,Novath Rukwago,akitoa maelezo jinsi Minziro day ilivyoanza na mpaka kufanikiwa.

 

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nkenge,Frolent Kyombo, aliwataka mipango inayoibuliwa na wana Minziro wanaoishi nje, wakawashirikisha wawakilishi wa wananchi ili kurahisisha kufikia maendeleo kwa haraka.

 

Aidha Waziri Mulamula, licha ya kuwapongeza aliwatia nguvu na kuwaasa kuiboresha zaidi shughuli hiyo ili iweze kuleta tija katika kata hiyo,  wilaya, mkoa wa Kagera na nchi kwa ujumla.

 

 

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Liberata Mulamula akiwa na Viongozi wa Kata ya Minziro, Wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera alipofika Katani hapo katika kuchangia Ujenzi wa bweni la Wasichana Shule ya Sekondari Minziro.

 

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Liberata Mulamula akipata maelezo ya Maendeleo ya Shule ya Sekondari Minziro toka kwa Mwalimu shuleni hapo.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Liberata Mulamula akizindua kitabu chenye historia nzima ya Kata ya Minziro Wilayani Misenyi mkoa wa Kagera.


Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Liberata Mulamula akiwa na viongozi mbalimbali wa Kata, Wilaya, Mkoa katika uchangiaji wa bweni la wasichana shule ya Sekondari Minziro.


Burudani zilitamalaki katika uchangiaji wa bweni la Wasichana katika shule ya sekondari Minziro, Ngoma hiyo inajulikana kwa jina la 'Mbutu' yenye asili ya Uganda ambayo ilikuwa kivutio kikubwa kwa wageni wote na wananchi walioshiriki katika maadhimish ya Minziro day.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso