Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akizungumza leo tarehe 29 Septemba 2026 mkoani Tabora wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na Kata 11 za Tanzania bara.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akizungumza leo tarehe 29 Septemba 2026 mkoani Tabora wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na Kata 11 za Tanzania bara.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima akizungumza jambo wakati wa mafunzo hayo.
Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Chamwino Mkoani Dodoma na Kata 11za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi**************Na. Mwandishi Wetu, Tabora
Watendaji wa uchaguzi wamesisitizwa kuheshimu viapo vyao na kutekeleza majukumu kwa kuzingatia Katiba, sheria na kanuni wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele leo tarehe 29 Septemba, 2026 mkoani Tabora wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi.
Mafunzo hayo ni sehemu ya mchakato wa maandalizi ya uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye Jimbo la Chamwino Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma na Kata 11 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika tarehe 04 Novemba, 2026.
“Ninawasisitiza kuheshimu viapo vyenu kwa nafasi mlizoteuliwa, tekelezeni majukumu yenu kwa kuzingatia Katiba ya Nchi, sheria za uchaguzi na kanuni zake, kanuni za maadili ya uchaguzi na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na yatakayotolewa na Tume katika kipindi hiki cha uchaguzi,” amesema Jaji Mwambegele.
Amewaelekeza watendaji hao kuhakikisha kuwa wakati wote wa mchakato wa uchaguzi huo, wanavishirikisha kwa karibu vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili na wadau wengine wa uchaguzi katika maeneo yao kuhusu masuala ya kiuchaguzi ambayo wanastahili kushirikishwa.
Ameongeza kuwa watendaji hao wanapaswa kuvipatia vyama vya siasa orodha ya vituo vya kupigia kura ili kuviwezesha kupanga mawakala.
“Ni muhimu kwenu pia, kuhakikisha mnayatambua na kuyajua vyema maeneo ambayo uchaguzi utaendeshwa ikiwemo miundombinu ya kufika katika vituo vya kupigia kura,” amesema Jaji Mwambegele.
Amewaasa watendaji hao kuhakikisha kuwa pamoja na uzoefu ambao baadhi yao wanao katika uendeshaji wa uchaguzi, wanaepuka kufanya kazi kwa mazoea kwa kuwa kila uchaguzi unatofautiana na uchaguzi mwingine.
Jaji Mwambegele amewasisitiza watendaji hao kuhakikisha wanaajiri watendaji wa vituo wenye sifa, weledi, wanaojitambua na kuachana na upendeleo kwa ndugu na jamaa ambao hawana sifa za kufanya shughuli za uchaguzi.
“Mhakiki vifaa vya uchaguzi mnavyopokea kutoka Tume na kuhakikisha kila mkuu wa kituo anapata vifaa vyote vya uchaguzi vinavyohitajika mapema na kuhakikisha siku ya uchaguzi mnaweka utaratibu utakaowezesha kila kituo cha kupigia kura kufunguliwa saa 1:00 asubuhi,” amesema.
Mafunzo hayo ya siku tatu yanawajumuisha waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na kata, maafisa uchaguzi, maafisa ununuzi na wahasibu.
Kata 11 za Tanzania Bara zitakazofanya uchaguzi wa Udiwani ni Nonde iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya; Lugenge, Halmashauri ya Mji Njombe; Bargish, Halmashauri ya Mji Mbulu; Makole, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza; Mwera, Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na Oldonyosambu, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
Nyingine ni Igalula iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Uyui; Shelui, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba; Mvumi, Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa; Nyarero, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na Ilolangulu, Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe.
Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Chamwino Mkoani Dodoma na Kata 11za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi
Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Chamwino Mkoani Dodoma na Kata 11za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.Naibu Msajili na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Tabora Mhe. Gabriel Patrick Ngaeje akiwaongoza washiriki wa mafunzo kula kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa pamoja na kutunza siri wakati wakitekeleza majukumu ya Uchaguzi.
Washiriki wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kutunza siri.






.jpeg)

.jpeg)
No comments:
Post a Comment