Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Dkt. Evaline Munisi, akisalimiana na Meneja Mkuu wa Barrick Bulyanhulu, Rhys Harvey, wakati wa mapokezi ya ujumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu. Katikati ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda, na pembeni ni Meneja wa Mahusiano ya Jamii na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu, Agapiti Paul.
Mwenyekiti wa Kudumu wa Kamati ya Bunge Ustawi na Maendeleo ya Jamii , Hawa Mchafu Chakoma akisalimiana na Meneja Mahusiano ya Jamii na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu , Agapiti Paul

Meneja Mkuu wa Barrick Bulyanhulu , Rhys Harvey akizugumza kwenye kamati hiyo ilipofanya ziara ya kikazi mgodi hapo.
Meneja Mkuu wa Barrick Bulyanhulu , Rhys Harvey akizugumza kwenye kamati hiyo ilipofanya ziara ya kikazi mgodi hapo.
Meneja Mahusiano ya Jamii na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu , Agapiti Paul akifanya wasilisho la utekelezaji wa sheria za kazi na usalama wa afya mahali pa kazi kwa kamati hiyo na matumizi ya teknolojia za kisasa.
Meneja Mahusiano ya Jamii na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu , Agapiti Paul akifanya wasilisho la utekelezaji wa sheria za kazi na usalama wa afya mahali pa kazi kwa kamati hiyo na matumizi ya teknolojia za kisasa.
Mwenyekiti wa Kudumu wa Kamati ya Bunge Ustawi na Maendeleo ya Jamii , Hawa Mchafu Chakoma akizungumza kwenye ziara hiyo , katikati ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi , Ajira na Mahusiano , Dkt. Evaline Munisi na wa kwanza kushoto ni Meneja Mkuu wa Barrick Bulyanhulu , Rhys Harvey.
Mwenyekiti wa Kudumu wa Kamati ya Bunge Ustawi na Maendeleo ya Jamii , Hawa Mchafu Chakoma akizungumza kwenye ziara hiyo umuhimu wa kuongeza mafunzo kwa wafanyakazi na wakandarasi wanaofanya kazi na mgodi huo kwa ajili ya usalama mahali pa kazi
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi , Ajira na Mahusiano , Dkt. Evaline Munisi akizungumza kwenye ziara hiyo
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi , Ajira na Mahusiano , Dkt. Evaline Munisi akizungumza kwenye ziara hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda akizungumza kwenye ziara hiyo.
Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakiwa katika picha ya pamoja
Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu
**
Kamati ya Kudumu ya Bunge Ustawi na Maendeleo ya Jamii imefanya ziara ya kikazi katika mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu na kupongeza jitihada zinazofanywa na mgodi kuzingatia kanuni za usalama mahali pa kazi,kujali afya za wafanyakazi wake na jamii nzima ya vijiji vinavyozunguka mgodi huo.
Pia kamati imepongeza uwekezaji mkubwa wa kampuni katika matumizi ya teknolojia za kisasa ambazo zimefanikisha kuwaweka wafanyakazi wake katika mazingira mazuri zaidi ya kufanyia kazi ambayo si hatarishi ya kusababisha matukio ya ajali na kuathiri afya za wafanyakazi wake.
Mwenyekiti wa kudumu wa kamati hiyo , Hawa Mchafu Chakoma, akiongea baada ya kuhitimisha ziara hiyo iliyofanyika Septemba 23,2026 amesema Kamati imeridhishwa kwa jinsi mgodi unavyotekeleza sheria za kazi , programu za afya na usalama mahali pa kazi.
“Tunawapongeza kwa kuwa kinara wa masuala ya usalama mahali pa kazi ambapo mwaka huu mmeshinda tuzo mbalimbali za OSHA.vilevile Katika wasilisho lenu tumeona ni jinsi gani kampuni ya Barrick iko mstari wa mbele kulinda afya za wafanyakazi wake na jamii nzima ya maeneo yanayozunguka mgodi na kwa jinsi inavyofanikisha miradi ya Afya kupitia fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) pia tumefurahi kusikia inavyotekeleza kwa vitendo sheria ya ushirikishwaji watanzania katika mnyororo wa thamani kwenye sekta ya madini (Maudhui ya Ndani ),”amesema Mhe. Chakoma.
Kwa niaba ya Kamati Mhe. Chakoma ametoa mapendekezo kuwa mgodi uhakikishe elimu ya Afya na Usalama inawafikia pia wafanyakazi wote na wakandarasi wote wanaofanya kazio na mgodi.
“Ni kweli kwenye wasilisho lenu tumeona hakuna kifo au ajali kubwa hata moja tangu mwaka huu uanze nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa kazi kubwa ila muhimu kwa wafanyakazi wote kupata mafunzo na kujengewa uwezo wa usalama na afya kwenye maeneo yao ya kazi,”ameongeza Mwenyekiti huyo wa Kamati ya maendeleo ya ustawi wa Jamii.
Chakoma ameeleza kuwa, mazingira mazuri ya kazi yanaongeza tija kwenye uzalishaji na kutengeneza wigo mpana zaidi kwa serikali kufanya kazi kwa pamoja na wawekezaji wa ndani na nje kwenye sekta ya madini nchini.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi , Ajira na Mahusiano, Dkt .Evaline Munisi ameupongeza Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kuwa kinara wa utekelezaji wa sheria za kazi , ajira , usalama na afya mahali pa kazi na umefanyiwa ukaguzi mwanzoni mwa mwaka huu na kukidhi viwango vya Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa kazi (OSHA) na kupatiwa Ithibati hali iliyopelekea mgodi ushinde tuzo saba za OSHA.
Ameongeza kuwa mgodi unatekeleza kwa viwango vya juu sheria za kazi, usalama na afaya mahali pa kazi ya sura 297 na umekidhi matakwa ya sheria hizo pamoja na wakandarasi wanaofanya kazi na mgodi huo.
Dkt. Munisi amesema Wizara hiyo kwa kushirikiana na OSHA imefanya kaguzi mbalimbali ambapo katika kipindi cha mwaka 2025/26 jumla ya kaguzi 871 zilifanyika na wafanyakazi 7,969 walipimwa afya zao katika Mkoa wa Shinyanga na waajiri 102 walikuwa wametekeleza sheria ya usalama na afya na kupatiwa leseni ya ithibati.
Awali akitoa taarifa kwa Kamati hiyo, Meneja Mahusiano ya Jamii na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu , Agapiti Paul amesema mgodi huo unafanikisha kwa vitendo sheria ya usalama mahali pa kazi kwa kutumia zaidi mashine , mitambo na teknolojia za kisasa (automation system) kwenye maeneo hatarishi chini ardhi kama vile upasuaji wa miamba , ulipuzi na uchorongaji wa miamba.
“Moja ya sera ya kampuni ya Barrick Bulyanhulu ni kuweka mbele afya ya wafanyakazi wake na tuna kauli mbiu kwamba unakuja kazini na kurudi nyumbani salama,” amesema Paul.
Paul ameeleza kuwa mbali na kuimarisha huduma za afya na usalama ndani ya mgodi pia umekuwa mstari wa mbele kuboresha kituo cha afya cha Bugarama na kupeleka kampeni ya kupambana na Malaria ijulikanayo kama ‘Zero Malaria’ kwenye vijiji vinavyozunguka mgodi kwa kupuliza dawa za kuua mazalia ya mbu na kuwagawia wananchi vyandarua vyenye dawa.
Ameongeza kwamba mgodi huo kupitia sera na kanuni ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kila mwaka unaendelea kutekeleza miradi mbalimbali kwenye maeneo ya afya , barabara , ujenzi wa mashule , mabweni na kilimo kwa kuwajengea uwezo vijana hasa wanaozunguka mgodi kupata shughuli za kujiingiza kipato.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama , Frank Nkinda ameshukuru Barrick Bulyanhulu kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kuwaletea wananchi maendeleo na kushirikiana na vijiji 16 vinavyozunguka mgodi huo kwa kuwapatia wanawake , vijana na makundi mbalimbali katika jamii nafasi ya kufanya kazi na mgodi huo ili kujikwamua kwenye umasikini wa kipato sambamba na uwekezaji wake kufanikisha miradi mikubwa ya maendeleo.


























No comments:
Post a Comment