ZIARA YA RAIS WA TAASISI YA DIASPORA KUFUNGUA MILANGO YA UTALII MAKUMBUSHO YA TAIFA LA TANZANIA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 27 August 2026

ZIARA YA RAIS WA TAASISI YA DIASPORA KUFUNGUA MILANGO YA UTALII MAKUMBUSHO YA TAIFA LA TANZANIA




Makumbusho ya Taifa la Tanzania imepokea ugeni mzito kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Diaspora wa Kiafrika (ADDI) ukiongozwa na Mwanzilishi na Rais wa taasisi hiyo, Balozi Dkt. Arikana Chihombori-Quao kutoka Zimbabwe, katika ziara maalum iliyofanyika tarehe 26 Agosti 2026 kwa lengo la kujifunza historia na urithi wa Tanzania.

Ziara hiyo inatajwa kuwa chachu kubwa katika kuimarisha diplomasia ya utamaduni na kutangaza utalii wa urithi, huku ikiiweka Makumbusho ya Taifa katika nafasi ya juu ya kuvutia wageni wenye asili ya Kiafrika kutoka mataifa mbalimbali duniani wanaotamani kujua chimbuko na utambulisho wao wa asili.

Ujio wa viongozi hao wa diaspora unazidi kuimarisha nafasi ya makumbusho hiyo kama kitovu kikuu cha utunzaji wa kumbukumbu za kihistoria, sambamba na kujenga daraja imara la kuwaunganisha Watanzania na ndugu zao waishio ughaibuni kupitia urithi wao wa pamoja.




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso