MBONI MHITA: SHINYANGA KUHAKIKISHA HAKUNA UHABA WA MADARASA, MADAWATI NA VITI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 20 August 2026

MBONI MHITA: SHINYANGA KUHAKIKISHA HAKUNA UHABA WA MADARASA, MADAWATI NA VITI

 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, amesema mkoa huo unaendelea kukagua na kuboresha miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo miradi ambayo Mwenge wa Uhuru utapita, huku akisisitiza kuhakikisha hakuna uhaba wa madarasa, viti, meza na madawati katika shule za mkoa huo.

Mboni amesema baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Mwanza, ameendelea na ziara pamoja na Kamati ya Usalama ya Mkoa kwa ajili ya kukagua miradi na kubaini maeneo yanayohitaji maboresho.

Amesema zoezi hilo linafanyika katika halmashauri zote sita za Mkoa wa Shinyanga na kata zote 130, kwa lengo la kuhakikisha kila mwanafunzi anapata mazingira bora ya kujifunzia.

“Tunapita na Kamati ya Usalama ya Mkoa kuhakikisha kwamba katika halmashauri zote sita za Mkoa wa Shinyanga na kata zote 130, hatuna uhaba wa madarasa, hatuna uhaba wa viti na meza, hatuna uhaba wa madawati,” amesema Mboni.

Ameongeza kuwa maeneo yenye changamoto yanaendelea kufanyiwa maboresho, ikiwemo ujenzi wa madarasa mapya na ukarabati wa yaliyopo, ili kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira salama na rafiki ya kujifunzia.

#MboniMhita #Shinyanga #MwengeWaUhuru #Maendeleo #Elimu #Madarasa #Madawati #ShinyangaKwanza

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso