Chalinze - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema, kati ya jambo ambalo halipaswi kuchezewa ni Muungano ambao unatakiwa kulindwa na kila mmoja maana ndio alama kubwa ya
Tanzania.
Mhe. Masauni ameyasema hayo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani katika ziara yake ya kikazi aliyoifanya Julai 22, 2026 akieleza kufurahishwa na shughuli za maendeleo katikaMkoa wa Pwani zinazofanyika ambazo zinaunganisha na Zanzibar ikiwemo bandari.
"Fursa ya Muungano inatakiwa kusaidia pande zote bara na Zanzibar na katika hili itakuwa inasaidia zaidi kwenye sekta ya utalii kwani mtalii anapokuja Zanzibar anaunganisha na Bagamoyo kwenye hifadhi ya Saadani",amesema.
Kadhalika amewataka vijana kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii katika kipindi hiki cha utandawazi kutokana na kuwepo kwa upotoshaji mkubwa unaofanywa na baadhi ya vijana.
Amewataka kutumia mitandao ya kijamii kwa mambo ambayo yatakuwa na faida kwao hususani kujifunza mbinu za kuboresha shughuli zao za kibiashara za kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Mbunge wa Chalinze ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Chalinzi inabadilika kwa kasi kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Serikali pamoja na wananchi wa eneo hilo.
Ameongeza kuwa ushirikiano baina ya viongozi na wananchi imesaidia kufanya kimbilio kwa wawekezaji wengi kutokana na kuwepo kwa miundombinu Rafiki jambo ambalo limeifanya Chalinze kukua kukua kila siku.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge alisema Wilaya ya Bagamoyo ni kati ya maeneo ya utalii ambayo kwasasa yanakuwa kwa kasi kwa kuwa na wawekezaji wengi wazawa na wageni wanaofika kuwekeza.
“Kuhusu suala la Muungano hapa Pwani watu wengi wanakutana na kufanya shighuli mbalimbali kutoka Zanzibar na Bagamoyo ni moja ya mji ambao wananchi wananufaika
na Muungano wa nchi yetu,”
Ameaema upo mpango wa ujenzi wa reli ya km 100 kutoka Bagamoyo kwenda bandari kavu ya Kwala ambayo itasaidia usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kutoka katika mji huo.
Mhe. Kunenge amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa barabara ya Afrika Mashariki ambayo itafungua wigo wa usafirishaji wa na Barabara ya Mlandizi Manerumango.
Amewataka wawekezaji kujenga hoteli kubwa za kitalii kwani uwekezaji huo unahitajika kwenye Wilaya hiyo ya kitalii ambayo kwasasa imekuwa na fursa nyingi za kimaendeleo.
Mkuu huyo wa Mkoa amemuomba Waziri Masauni kufikisha ombi la Halmashauri ya Chalinze kuwa Manispaa kutokana na kuwa na vigezo vingi kikiwemo cha ongezeko la kukua kwa mapato.

No comments:
Post a Comment