Wito umetolewa kwa vijana nchini kuendelea kuwa kielelezo cha utulivu, umoja na mshikamano, huku wakisisitizwa kutambua kuwa maendeleo hayawezi kupatikana bila kuwepo kwa amani na utulivu katika jamii.
Akizungumza Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera, Faris Buruhan, amesema vijana wana wajibu mkubwa wa kuilinda Tanzania na kudumisha mshikamano wa kitaifa.
“Tanzania ni yetu, tunawajibika kuilinda na hatupaswi kukubali watu watuchonganishe. Tusikubali kuharibu ustawi na amani ya nchi yetu, kwa sababu maendeleo yoyote yanapatikana katika mazingira yenye utulivu,” amesema Faris.
Aidha, amewahimiza vijana kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kujiongezea kipato na kuboresha maisha yao, akibainisha kuwa kipindi cha uchaguzi kimekwisha na sasa ni wakati wa kujikita katika shughuli za maendeleo kwa manufaa ya taifa.

No comments:
Post a Comment