📌Aipongeza TANESCO kuendelea kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa umeme.
📌Ahimiza TANESCO kuendelea kupanda miti kwa wingi kwenye vyanzo vya uzalishaji wa umeme
Na. Mariam Juma, Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kwagilwa Reuben leo Juni 01, 2026 ametembelea banda la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwenye Maonesho kuelekea Siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Center (JKCC) Jijini Dodoma.
Akizungumza katika banda hilo Mhe. Kagilwa ameipongeza TANESCO kwa jitihada kubwa wanazozifanya katika utunzaji wa Mazingira hasa katika kuendelea kuhamasisha wananchi kupika kwa kutumia Nishati Safi ya umeme hali ambayo inasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira.
Aidha ametumia nafasi hiyo kuisisitiza TANESCO kuendelea kupanda miti kwa wingi kwenye vyanzo vya uzalishaji wa umeme ili kuendelea kutunza mazingira.
" Niwapongeze TANESCO kwa kuendelea kuhamasisha utunzaji wa mazingira hususani kupitia Nishati Safi ya kupikia kwa umeme, pia niwasisitize kuongeza juhudi za upandaji miti kwenye vyanzo vya uzalishaji wa umeme".
Awali akielezea ushiriki wa TANESCO katika maonesho hayo Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja Mkoa wa Dodoma James Vesso amesema lengo ni kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa umeme hali inayosaidia kuokoa muda na kutunza mazingira.
"Sisi kama TANESCO tunaendelea kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kutumia Nishati Safi ya kupikia kwa umeme ili kutunza mazingira pamoja na kueleza mikakati ya Shirika juu ya utunzaji wa mazingira katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme"









No comments:
Post a Comment