MCHUNGAJI ISAYA DANIEL AHIMIZA KUREJEA MAADILI YA KIUNGU KAMA NJIA YA KULINDA AMANI YA TANZANIA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday, 19 April 2026

MCHUNGAJI ISAYA DANIEL AHIMIZA KUREJEA MAADILI YA KIUNGU KAMA NJIA YA KULINDA AMANI YA TANZANIA







Na Mwandishi Wetu


Mchungaji Isaya Daniel wa Kanisa la FPCT Mhongolo amewataka Watanzania kurejea katika misingi ya kumcha Mungu, kuheshimiana na kusameheana ili kuendelea kuilinda amani ambayo taifa limejivunia kwa zaidi ya miaka 60.


Akizungumza leo katika ibada kanisani hapo, Mchungaji Isaya amesema amani ya Tanzania haikujengwa kwa bahati mbaya, bali ilitokana na maadili mema, upendo wa kweli na mshikamano uliorithishwa kutoka kizazi hadi kizazi.


Amesema katika miaka ya nyuma jamii ilikuwa na utamaduni wa kusikilizana, kuheshimu wakubwa na kuishi kwa kujali wengine, jambo lililosaidia kuondoa migogoro isiyo ya lazima.


Kwa mujibu wa mchungaji huyo, hofu ya Mungu ilikuwa nguzo muhimu iliyowaongoza watu kufanya yaliyo mema na kujiepusha na chuki, ubaguzi na matendo yanayoweza kuvuruga umoja wa taifa.


“Mtu anayemcha Mungu hawezi kufurahia kuona mwenzake anaumia, Upendo wa Mungu unatufundisha kuishi kwa amani na watu wote,” ameeleza.


Akinukuu mstari wa biblia kitabu cha Waebrania 12 na mstari wa 14 unasema kuwa,
"Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao."


Mchungaji Isaya pia amewataka wazazi, viongozi wa dini na jamii kwa ujumla kushirikiana katika malezi ya watoto kwa kuwajenga katika maadili ya heshima, ukweli na uwajibikaji.



Mchungaji Isaya Daniel amesema amani ni tunu ya taifa inayopaswa kulindwa kwa matendo ya kila siku kupitia upendo, subira na maridhiano.


#HekimaYetu #TanzaniaTulivu

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso