WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Aprili 19, 2026 ameweka jiwe la msingi la Mradi wa Maji wa Miji 28 katika mji wa Chamwino mkoani Dodoma.
Mradi huo wa kimkakati wenye thamani ya Shilingi bilioni 17.20, unatekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) na mpaka sasa umefikia asilimia 70.2 ya utekelezaji.
Kukamilika kwa Mradi huo kutawezesha kuhudumia zaidi ya wananchi 60,000 katika kata za Msanga, Buigiri, Chamwino na Mtumba, na kuongeza upatikanaji wa maji safi kutoka asilimia 91 hadi 100 pamoja na kuimarisha uzalishaji wa maji kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye.
Akizungumza katika tukio hilo, Waziri Mkuu alimpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa mradi huo mkubwa ambao utanufaisha wakazi wa Wilaya ya Chamwino.




No comments:
Post a Comment