SALOME MAKAMBA AZIAMSHA TAASISI ZA FEDHA, KUSAIDIA VIJANA WABUNIFU NISHATI SAFI - HUHESO DIGITAL BLOG
  • Home
  • About
  • Contact

HUHESO DIGITAL BLOG
    • Features
    • _Multi DropDown
    • __DropDown 1
    • __DropDown 2
    • __DropDown 3
    • _ShortCodes
  • Breaking

    Post Top Ad

    Friday, 6 February 2026

    Home HABARI SALOME MAKAMBA AZIAMSHA TAASISI ZA FEDHA, KUSAIDIA VIJANA WABUNIFU NISHATI SAFI

    SALOME MAKAMBA AZIAMSHA TAASISI ZA FEDHA, KUSAIDIA VIJANA WABUNIFU NISHATI SAFI

    NKUMBI 15:01 ,HABARI


    Serikali imezitaka taasisi za fedha nchini kuelekeza nguvu na uwekezaji kwa wajasiriamali pamoja na wabunifu wa kidijitali waliojikita katika biashara ya nishati ili kuharakisha utekelezaji wa ajenda ya taifa ya kuhakikisha asilimia 80 ya wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

    Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema wakati wa uzinduzi wa mradi wa nishati safi katika shule ya sekondari ya wasichana ya Bunge iliyopo mkoani Dodoma, ingawa matumizi ya nishati safi yameongezeka kutoka asilimia 6.9 mwaka 2021 hadi asilimia 23.2 mwaka 2025, bado kuna safari ndefu ya mafanikio kwani takribani asilimia 77 ya kaya bado zinatumia nishati isiyo safi.

    Naibu Waziri amewasisitiza wasambazaji wa gesi ya mitungi kuongeza vituo vya usambazaji na ujazaji ili kurahisisha upatikanaji wa nishati hiyo kwa wananchi wengi zaidi, huku akiwahamasisha wabunifu na vijana walioko vyuoni kufanya tafiti na kubuni teknolojia zitakazorahisisha usambaaji wa ajenda hiyo nchi nzima.

    Mradi huo uliomalizika shuleni hapo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la serikali linalozitaka taasisi zinazohudumia watu zaidi ya 100 kutumia nishati safi ili kulinda afya za binadamu na kutunza mazingira, hatua inayokwenda kuokoa gharama kubwa kwani shule hiyo yenye wanafunzi 555 imekuwa ikitumia wastani wa shilingi milioni 10.5 kila baada ya miezi mitatu kwa ajili ya ununuzi wa kuni pekee.
    Tags HABARI#
    Share This
    Author Image

    About NKUMBI

    HABARI
    by NKUMBI at 15:01
    Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
    Tags: HABARI

    No comments:

    Post a Comment

    Newer Post Older Post Home
    Subscribe to: Post Comments (Atom)

    Post Top Ad

    Author Details

    Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

    Kilele Foundation Kenya

    RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
    Powered by Blogger.

    WANAOTUFUATA

    SUPPORTING LIVESTRONG

    SUPPORTING LIVESTRONG

    PARTNERSHIP NUTRITION IN TANZANIA

    PARTNERSHIP NUTRITION IN TANZANIA

    JOIN US TO CLIMB KILIMANJARO FOR EAST AFRICA OUTREACH FOR WOMEN.

    JOIN US TO CLIMB KILIMANJARO FOR EAST AFRICA OUTREACH FOR WOMEN.
    Please support our cause to climb Kilimanjaro for East Africa Outreach for Women, Join us to support small business in East africa.

    TANZANIA

    TANZANIA

    Mount Kilimanjaro in Tanzania

    Mount Kilimanjaro in Tanzania

    KAHAMA IN TANZANIA

    KAHAMA IN TANZANIA

    Welcome in Tanzania.

    Welcome in Tanzania.

    POPULAR HUHESO BLOG

    • NGOMA MPYA YA KISIMA MAJABALA - KARIBU
        Pata nafasi kumsapoti Kisima katika video yake mpya iitwayo Mele Mpya Itwayo Mele Ni Ngoma Kali  Kisima Majabala_Song_Mele Director_Migera...
    • GUDE GUDE NA WIMBO WAKE MPYA WA SHIDA
       Usipite bila kuangalia ngoma kali ya Gudegude iitwayo shida
    • VIJANA WAJITENGA NA MAANDAMANO, WAAPA KULINDA AMANI UCHAGUZI MKUU
      Vijana wa Wilaya ya Kahama wakiwa katika kongamano lao lililofanyika viwanja vya magereza - Kahama, kwa lengo la kutoa tamko la vijana wa Ka...
    • WAGOMBEA 16 WA UBUNGE WACHUKUA FOMU KATIKA MAJIMBO YA KAHAMA
      NA NEEMA NKUMBI HUHESO DIGITAL KAHAMA Juni 28, 2025 – Kahama Jumla ya wagombea 16 wa nafasi ya ubunge kutoka katika majimbo matatu ya Wilaya...
    • TUME YATOA RATIBA MPYA, SAU, CUF, ACT WAZALENDO NAO KUCHUKUA FOMU ZA URAIS
       

    Subscribe Huheso Digital Blog

    Posts
    Atom
    Posts
    Comments
    Atom
    Comments

    Pages

    • Home

    CONTACT US

    • (HUHESO Digital Blog
    • NKUMBI

    EXECUTIVE DIRECTOR

    EXECUTIVE DIRECTOR
    JUMA MWESIGWA

    CHUO

    CHUO

    HUHESO FOUNDATION

    NON GOVERMENTAL ORGANIZATION

    Found in the year 2009 as supportive group of Children, Youth,Women and disabled group
    especially people with special need families. The group was serving the neediest families
    affected by HIV/AIDS and CANCER. The Foundation for Human Health society is a Foundation of marginalized people
    and community based organizations dealing with HIV/AIDS issues human rights abuse,Cancer,Breast Cancer,
    reproductive health to adolescents/youth and empowerment of women in TANZANIA.

    Labels

    BURUDANI NA MICHEZO HABARI HUHESO FOUNDATION JOB OPPORTUNITY MAGAZETI MATANGAZO YA TENDA MATUKIO MICHEZO NEWSPAPER SIASA

    ALL VISTORS COUNTER

    Copyright © HUHESO DIGITAL BLOG
    Huheso