RAIS SAMIA ATOA POLE KUFUATIA KIFO CHA BW. CHARLES HILARY, MKURUGENZI WA MAWASILIANO IKULU ZANZIBAR - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday, 11 May 2025

RAIS SAMIA ATOA POLE KUFUATIA KIFO CHA BW. CHARLES HILARY, MKURUGENZI WA MAWASILIANO IKULU ZANZIBAR

 


Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Bw. Charles Hilary, Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu Zanzibar kilichotokea leo Mei 11, 2025.


Ninatoa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi, familia, ndugu, jamaa na marafiki na wadau wote wa sekta ya habari nchini kwa msiba huu.


Ndugu Charles Hilary atakumbukwa kwa mchango wake adhimu wa zaidi ya miaka 40 katika kukuza sekta ya habari nchini tangu akiwa redioni hadi kwenye televisheni, pamoja na unasihi kwa wanahabari wachanga.


Namuomba Mwenyezi Mungu aijaalie familia yake uvumilivu na subra katika kipindi hiki kigumu, na ailaze roho ya mpendwa wetu mahala pema.


Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake tutarejea.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso