CCM KAHAMA YATOA ONYO KALI KWA WATIA NIA WANAOTOA RUSHWA KABLA YA MCHAKATO RASMI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 9 May 2025

CCM KAHAMA YATOA ONYO KALI KWA WATIA NIA WANAOTOA RUSHWA KABLA YA MCHAKATO RASMI

 

Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama Andrew Chatwanga akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi yake Kahama.


Na Neema Nkumbi - Huheso digital Kahama, Shinyanga


Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama kimewatoa onyo kali kwa wanachama wanaotia nia ya kugombea nafasi za udiwani na ubunge, wanaoanza kampeni za chinichini kwa kutoa hongo kwa wajumbe kabla ya mchakato rasmi wa uchaguzi kuanza.


Akizungumza na waandishi wa habari may 8, 2025 Katibu wa CCM Wilaya ya Kahama, Ndg. Andrew Chatwanga, amesema kuwa chama kimepokea taarifa za kuwepo kwa baadhi ya watia nia wanaowaita wajumbe wa mkutano mkuu na kuwapa fedha kiasi cha shilingi elfu kumi kwa kila mmoja, kitendo ambacho ni kinyume na maadili, kanuni na taratibu za chama hicho.


"Chama cha Mapinduzi kimeweka utaratibu mzuri sana wa kugombea, lakini baadhi ya watia nia wameanza kutoa hongo kwa wajumbe, hiyo siyo CCM tunayoitaka. Kuwapa watu elfu kumi ni kuwadhalilisha wanachama wetu na kudhoofisha taswira ya chama," amesema Chatwanga.




Chatwanga amefafanua kuwa mchakato rasmi wa kugombea utaanza kwa kuchukua fomu, kisha kufuatiwa na vikao halali vya chama ambavyo vitapitia majina ya wagombea na hatimaye kuwasilisha majina matatu kwa Kamati Kuu ya Taifa kwa ajili ya uteuzi.


“Watu wanaweza kuchukua fomu hata mia moja, lakini mwisho wa siku ni majina matatu pekee yatakayochaguliwa na kupelekwa kwa ajili ya kura za maoni, Rushwa si kigezo cha kupata nafasi katika CCM. Kiongozi bora ni yule anayeishi na wananchi, anayejua matatizo yao na anayetambulika kwa uadilifu," ameongeza Chatwanga.


Aidha, amewataka wale wote wanaofanya mikutano ya siri usiku na kutoa fedha kwa wajumbe kuacha mara moja, akisema chama kina taarifa na majina yao yote hivyo hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kukiuka taratibu hizo.


"Chama kitachukua hatua kali kwa wale wote wanaokiuka maadili, Ubunge na udiwani ni nafasi za uwakilishi, si biashara ya fedha, Tunataka wagombea wanaotokana na mapenzi ya wananchi, si wale wanaonunua nafasi kwa njia ya rushwa," amesema Chatwanga.


Katibu huyo amesisitiza kuwa wabunge waliopo madarakani waachwe wafanya kazi zao hadi muda wao utakapomalizika, na kwamba vitendo vya hujuma na mikakati ya kuwahujumu havitavumiliwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso