WAZIRI MKUU AWATAKA VIJANA KUACHA KUTUMIA BANGI NA MIRUNGI ILI KUNUSURU MAISHA YAO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 2 April 2024

WAZIRI MKUU AWATAKA VIJANA KUACHA KUTUMIA BANGI NA MIRUNGI ILI KUNUSURU MAISHA YAO


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema dawa za kulevya aina ya bangi na mirungi zimendelea kutumiwa kwa wingi hapa nchini.

Amesema hayo leo Aprili 2, 2024 katika sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Kilimanjaro.

"Hivi karibuni kumeibuka aina nyingine ya bangi yenye kiasi kikubwa cha kilevi inayofahamika kama cha ‘Arusha na Skanka’ aina hii ya bangi yenye sumu nyingi huchanganywa kwenye sigara, lakini ukishaitumia watumiaji hubadilika na kuwa vichaa.

“Ni wakati mzuri sasa kwa vijana ambao ni watumiaji wa cha ‘Arusha na Skanka’ kuacha ili waweze kunusuru maisha yao kwa kuwa wanaitajika katika Taifa hili,"amesema Majaliwa

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso