ASHA AHUKUMIWA JELA MAISHA KWA KUMBAKA MVULANA WA MIAKA 15 MTWARA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 4 April 2024

ASHA AHUKUMIWA JELA MAISHA KWA KUMBAKA MVULANA WA MIAKA 15 MTWARA

Mahakama ya Wilaya ya Mtwara imemhukumu kifungo cha maisha jela, Asha Ismail Chanchoni (47) kwa kosa la shambulio la aibu, baada ya kujihusisha kimapenzi na mvulana mwenye umri wa miaka 15.



Hukumu hiyo imetolewa Aprili 2, 2024 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Lucas Jang’andu aliyesema Mahakama imethibitisha bila kuacha shaka kuwa mwanamke huyo alikuwa akijihusisha kimapenzi na mvulana huyo.

Kulingana na ushahidi uliotolewa mahakamani na mashahidi wawili wa upande wa Jamhuri, tukio hilo lilitokea Februari 2023 katika mtaa wa Chuno katika manispaa ya Mtwara Mikindani anakoishi mwanamke huyo.

Akichambua ushahidi, Hakimu Jang’wandu alisema siku ya tukio mshtakiwa alimbaka mtoto huyo kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kutoka kwa mashahidi mawili.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso