ZUCHU AOMBA RADHI BAADA YA KUFUNGIWA ZANZIBAR - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 6 March 2024

ZUCHU AOMBA RADHI BAADA YA KUFUNGIWA ZANZIBAR



Msanii, Zuhura Othman Masoud maarufu Zuchu ameomba radhi mashabiki wake na jamii kwa ujumla baada ya kufungiwa na Baraza la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni la Zanzibar, kuendesha shughuli zote za sanaa visiwani Zanzibar.


(Imeandaliwa na Mwandishi Wetu)

Zuchu ameomba radhi leo Jumatano Machi 6, 2024 baada ya hapo jana kuitwa na Baraza la Sanaa la Tanza-nia (Basata) waliofanya naye kikao huku akitoa shukrani zake kwa baraza hilo.


Mbali na kuendesha shughuli za sanaa, pia redio na televisheni za Zanzibar, zimepigwa marufuku kucheza nyimbo zake zote kwa kipindi cha miezi sita.


Hatua hiyo ilikuja baada ya tukio la Februari 24 mwaka huu wakati msanii huyo akitumbuiza katika usiku wa Fullmoon Kendwa Mkoa wa Kaskazini Unguja kudaiwa kuimba nyimbo, kutoa matamshi na kuonyesha ishara mbaya ambazo ni kinyume na maadili ya Kizanzibari.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso