WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KUTAMBUA MAENEO YAO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 6 March 2024

WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KUTAMBUA MAENEO YAO


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewataka wananchi wa wilaya ya Mbulu mkoani Manyara kujitokeza kwa wingi kuomba maeneo yao ya ardhi kutambuliwa.



‘’Naomba muendelee kujitokeza kwa wingi ili maeneo yenu yatambuliwe na hii itasaidia sana wanachi wa Mbulu kutogombana katika masuala ya ardhi kwa kuwa kila mmoja atakuwa na hati yake’’. Amesema Mhe, Pinda


Mhe, Pinda ametoa kauli hiyo tarehe 5 Machi 2024 katika halmashauri ya mji wa Mbulu wakati wa zoezi la kutoa hati kwa wananchi waliotambuliwa kupitia mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha (KKK) akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani Manyara.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso