WATATU WAUAWA NA ANAYESADIKIKA KUWA MGONJWA WA AKILI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 15 March 2024

WATATU WAUAWA NA ANAYESADIKIKA KUWA MGONJWA WA AKILI

Watu watatu wameuwawa akiwemo mama mjamzito wa miezi 7 huku mtuhumiwa akidaiwa kuwa na matatizo ya Afya ya akili ambapo tukio hilo limetokea kata ya Sirop Wilayani Hanang mkoani Manyara siku ya tarehe 13 march mwaka huu.



Kamanda wa jeshi la polisi SACP George Katabazi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo,ambapo amesema waliouwawa ni mama mzazi wa mtuhumiwa, mama wa jirani ambaye ni mjamzito wamiezi 7 pamoja na mtoto wake wa mwaka Mmoja.


Aidha Kamanda SACP Katabazi amesema chanzo cha tukio hilo ni matatizo ya Afya ya akili aliyokuwanayo mtuhumiwa na mpaka sasa anashikiliwa na jeshi hilo kwa uchanguzi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso