WADAU WA MSD WAHIMIZWA MATUMIZI SAHIHI YA TAKWIMU ZA UGAVI WA BIDHAA ZA AFYA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 22 March 2024

WADAU WA MSD WAHIMIZWA MATUMIZI SAHIHI YA TAKWIMU ZA UGAVI WA BIDHAA ZA AFYA

 

Wadau wa afya wa Bohari ya Dawa,MSD Mtwara wamehimizwa kusimamia matumizi sahihi ya takwimu za mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya, ili ziwawezeshe kufanya maamuzi sahihi juu ya bidhaa hizo katika maeneo yao.

Akifungua kikao cha wadau na wateja wa MSD kanda ya Mtwara, Mkuu wa Wilaya ya Masasi Lauteri Kanoni amesema uwepo wa takwimu sahihi unaiwezesha MSD kuagiza kwa usahihi bidhaa za afya na kuboresha upatikanaji wa bidhaa hizo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.


Aidha, amewashauri MSD kuhakikisha utaratibu wa vikao vya mwaka vya wadau ni muhimu kwa pande zote mbili, yaani Bohari ya Dawa (MSD) yenyewe na wadau ili kwa pamoja kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya, kwa kujadili changamoto na kuzitafutia utatuzi.


Kwa upande wake Meneja Kanda ya Mtwara Tea Malay ameeleza kuwa kwa sasa kanda ya MSD Mtwara inahudumia vituo vya kutolea huduma za afya 631, na inasambaza bidhaa za afya kila baada miezi miwili.


Naye Meneja Huduma kwa Wateja na Miradi Dkt. Pamella Sawa ameeleza kuwa vikao vya MSD na wadau wake kuanzia sasa vitakuwa endelevu kila mwaka.


MSD Kanda ya Mtwara inahudumia mikoa ya Lindi,Mtwara na Wilaya ya Tunduru.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso