STEVE NYERERE AFICHUA MPANGO WA KUMWEKEA SUMU ULIVYOSUKWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 14 March 2024

STEVE NYERERE AFICHUA MPANGO WA KUMWEKEA SUMU ULIVYOSUKWA


Jina lake wengi walianza kulifahamu kutokana na kuigiza sauti za viongozi mbalimbali huku ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere na mwanasiasa Augustine Mrema, ikiwa imekubalika zaidi kwa mashabiki wake hadi kumpatia jina la Steve Nyerere, licha ya kuwa jina halisi ni Steve Megele.



Licha ya kuwa wapo wanaompenda kutokana na vipaji vyake vya kuburudisha Steve amedai kuwa anakumbana na changamoto ya kuchukiwa, huku akisimulia alivyonusurika kifo mwaka 2015, baada ya kuwekewa sumu kwenye chakula.


Steve akiendelea kusimulia tukio hilo, amedai baada ya kutokea tukio hilo mpishi wa eneo hilo alikwenda kumuomba msamaha na kueleza tukio lilivyokuwa.


Amedai kuwa kuna mtu alitumia njia ya uongo kumdanganya mpishi wakati anaandaa chakula, kwa kumwambia kuwa ameagizwa na Steve kuweka kitu kwenye chakula kwa ajili ya kuongeza ladha na hamu ya kula, hivyo mpishi alikubali na kuweka kitu hicho bila ya kujua ilikuwa sumu.


“Mpishi wa eneo lile aliomba msamaha, baada ya kuulizwa na vijana wangu alisema alipelekewa kitu na mtu asiyemfahamu akamwambia kuwa yupo na mimi, hivyo nimemuagiza ampe kitu kile ili aniwekewe kwenye chakula kwa ajili ya kuongeza ‘apitaiti’.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso