SINA TATIZO NA ZUCHU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 21 March 2024

SINA TATIZO NA ZUCHU


Zarina Hassan ambaye ni Mama Watoto wa Mwimbaji Diamond Platnumz, amewasili Tanzania usiku wa kuamkia leo March 21,2024 na asubuhi hii ameongea na Waandishi wa Habari kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo ukaribu wake na Msanii Zuchu ambaye amesema ni Mtu mzuri na hata Watoto wake wakiwa Tanzania huwa kwenye mikono salama na huwa anawasiliana na Zuchu kujua maendeleo yao.



Zari amesama hayo wakati akisaini mkataba mwingine na Kampuni ambayo amekuwa akifanya nayo kazi kwa zaidi ya miaka mitatu ambapo amesema “Nimekuwa nikifanya kazi vizuri na kampuni hii, wamefurahia kuongeza mkataba na Mimi ambaye brand yangu imezidi kuwa kubwa Afrika Mashariki”

Kuhusu uhusiano wake na Diamond na Wazazi wenza,
Zari amesema “Watu wanachukuliaga eti Mimi siongei na Wanawake wa Diamond, naongea na Zuchu hata kama Watoto wanakuja Tanzania simtafuti hata Baba T (Baba Diamond) hata kumwambia eeh jamani kinachojiri, nampigia Zuchu namwambia hey za asubuhi mnaendeleaje atajibu aah tunafanya hivi tunaenda swimming, kwasababu sioni tatizo kwanza Zuchu Mtu mzuri sana na Watoto wangu wakiwa huku wanakuwa na utulivu kabisa kuwa na yeye”

“Kuhusu Mtoto wa Hamisa Diamond mwenyewe atajielezea kama Mtoto wake ama sio wake Mimi sijui, akiniambia huyu ni Mtoto wangu nataka ajuane na hawa wangu nitamkaribisha”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso