LAAC WASHTUKIA UPIGAJI FEDHA UJENZI WA HOSPITALI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 21 March 2024

LAAC WASHTUKIA UPIGAJI FEDHA UJENZI WA HOSPITALI


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imetoa maelekezo kwa watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo waliosimamia mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya na kusema kuwa kamati hiyo haijaridhishwa na usimamizi wa mradi huo na dalili zinaonesha waziwazi kuna ubadhirifu wa fedha.



Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya LAAC, Ester Bulaya akiwa na wajumbe wa kamati baada ya kukagua ujenzi wa mradi wa hospitali ya Wilaya ya Rombo na baadae kukagua mradi wa jengo la halmashauri.


Bulaya amesema lengo la kamati ya LAAC ni kuangalia matumizi ya fedha za umma na ubora wa kazi zilizofanyika katika halmashauri ambapo ameeleza kusikitishwa kwa miradi ya Halmashauri ya Wilaya ya Rombo kwa kuchukua muda mrefu, kutokukamilika kwa muda wakati Serikali ilishawapatia fedha za kutekeleza miradi hiyo.


Akieleza kuonekana kwa dalili za ubadhirifu wa fedha zilizotumika katika ujenzi wa hospitali ya wilaya amesema, maelekezo yalitolewa na Serikali na miongozo ya Ofisi ya TAMISEMI ni kuwa Sh milioni 800 zilitakiwa kujenga majengo manne na badala yake yamejengwa majengo mawili pamoja na halmashauri kuongeza fedha kutoka mapato ya ndani zaidi ya Sh milioni 170 lakini pia fedha hizo hazionekani matumizi yake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso