SHAMBA LA CHANGANYWA BANGI, MAHINDI NA ALIZETI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 7 March 2024

SHAMBA LA CHANGANYWA BANGI, MAHINDI NA ALIZETI

 
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini wamefanikiwa kuteketeza zaidi ya ekari 50 za bangi eneo la Kisimiri wilayani Arumeru, ambazo zilikuwa zimepandwa kwa kuchanganywa na mazao mengine ya chakula kama mahindi, maharage na alizeti.




Akizungumza wakati wa tukio la kufyeka na kuchoma moto likiendelea mkuu wa operesheni-DCEA Kanda ya Kaskazini, Innocent Masangula amesema kwa makadirio ni zaidi ya gunia 350 za bangi zimeteketezwa kwenye mashamba hayo.


Kwa upande wake Ofisa Elimu wa Mamlaka hiyo, Shabani Miraji licha ya kuwakumbusha madhara ya dawa hizo amesisitiza namna kilimo hicho kinavyohatarisha usalama wa mazao ya chakula.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso